WEKEZA KATIKA UCHIMBAJI MADINI YA TANZANIA
Wizara ya Madini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikishirikiana na dmg events na Ocean Business Partners Tanzania, inayofuraha kukutangazia kuwa mkutano unaofuata wa Jukwaa la Madini na Uwekezaji Tanzania utafanyika Dar Es Salaam kuanzia 25 – 26 Oktoba 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Jukwaa hili limeandaliwa chini ya Uongozi wa Muheshimiwa Anthony Peter Mavunde, Waziri wa Madini, pamoja na wawakilishi kutoka ngazi za juu serikalini.
Kauli mbiu ya Jukwaa la Madini na Uwekezaji Tanzania 2023 “Kufungua uwezo wa baadaye wa uchimbaji wa madini Tanzania” kwa mara nyingine tena utawaunganisha wadau watanzania, na wengine kutoka bara la Afrika na kwingineko duniani pamoja na Mawaziri, Wakurugenzi Wakuu, Watunga sera, na viongozi katika tasnia ya madini jijini Dar Es Salaam ili wakutane na kujadili ana kwa ana mikakati ya ushirikiano itakayowezesha kufungua na kusukuma mbele maendeleo makubwa katika sekta hii muhimu.
WATOA MADA WA KIWIZARA, SERIKALI KUU, NA KITASNIA
KUHUSU MKUTANO KWA UFUPI
Maonensho
Imevutia zaidi ya washiriki 2,000 kutoka nchini kote Tanzania, Afrika na kwingineko duniani ili kuleta fursa baina ya serikali na wafanyabiashara (G2B) na wafanya biashara baina yao (B2B kwa lengo la kukuza minyororo ya thamani ya madini moja kwa moja kutoka kwenye migodi hadi sokoni.
Mkutano
Kujadili fursa ya Tanzania katika kujenga na kukuza nafasi yake kama kitovu cha biashara ya madini katika Afrika ya Mashariki na kufika duniani kote kutokana na shughuli zake za utafutaji na uchimbaji wa madini huku ikiunga mkono juhudi za kuhamia katika uchumi wa kijani.
Udhamini
Weka kampuni yako katika nafasi nzuri ya kuwa mbia wa wadau wote wanaoshiriki katika biashara ya kimataifa ya madini Tanzania na uwe leo sehemu ya historia ya Jukwaa la Madini na Uwekezaji Tanzania